Msanii wa muziki Gift Stanford maarufu kama, Gigy Money aliyefanya vizuri na kibao chake cha ‘Papa’ baada ya kimya kirefu ameachia ngoma yake mpya inayoenda kwa jina la ‘kiki’ aliyomshirikisha msanii Whozu na Sanja.

Katika wimbo huo Gigy amekuja na miondoko tofauti ya kuimba ambapo ameimba kwa kuchana tofauti na ilivyozoeleka, alipofanyiwa mahojiano na moja ya chombo cha habari hapa jijini Dar es salaam, Gigy amesema ameamua kuchana kutokana na kuzikubali kazi za malkia wa michano nchini Marekani, Card B hivyo ameamua kuiga miondoko.

Aidha siku chache zilizopita Gigy Money ame-make headlines nyingi katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii upande wa burudani baada ya kuingia katika migogoro na watu mbalimbali,  ukiwemo ule wa kuachana na baba mtoto wake, Moj360 mashabiki wamedhani ni moja ya kiki ya kusogeza  wimbo wake mpya wa Kiki.

Bofya kitufe chekundu hapa chini kuutazama wimbo huo na kumuona Gigy Mapesa akiRAP.

LIVE: Ndege mpya ya Tanzania Boeing 787-8 Dreamliner ikiwasili
Jeshi la Polisi kufanya operesheni kali visiwa vya viwa Viktoria

Comments

comments