Muimbaji wa muziki wa Injili nchini, Goodluck Gosbert amezungumzia furaha aliyokuwa nayo baada ya kualikwa Ikulu na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na kutumbuiza.

Goodluck amesema kuitwa Ikulu na kuimba mbele ya rais Magufuli ni jambo kubwa na limeweka historia katika maisha yake.

‘’Nilipigiwa simu, simu ilitoka Ikulu Streight (moja kwa moja) ikanifikia mimi kwa bahati nzuri au mbaya sikuwa na simu karibu akapigiwa meneja wangu bwana mnaitajika,” amesema Goodluck

Aidha, mwezi Aprili mwaka huu Rais Magufuli wakati wa uzinduzi wa mradi wa umeme Kinyerezi awamu ya pili aliusifia wa wimbo wa msanii huyo.

 

 

Ni vita ya Man Utd Vs Tottenham Hotspurs
Makonda awaonya watakaonunua makontena yake