Msanii wa nyimbo za injili, Goodluck Gozbert ameeleza jinsi ambavyo amekuwa akisaidia kuwainua wasanii wachanga kwenye tasnia ya muziki wa injili kwa hali ya kipekee.

Akifunguka katika mahojiano maalum na Dar24, mkali huyo wa ‘Ipo Siku’ ameeleza kuwa amekuwa akiwapa nafasi wasanii wanaochipukia kwenye albam zake ili kuwaweka moja kwa moja kwenye uso wa mkondo mkuu wa muziki huo.

Amesema katika albam yake mpya ya ‘Shukurani’, amewashirikisha wasanii wapya ambao wana uwezo mkubwa na wameuonesha ndani ya kazi hizo.

“Kwenye hii albam yangu nimewaweka chipukizi, yaani kolabo niliyoifanya nimefanya na wasanii chipukizi. Kabla ya hapo mimi sikuwahi kufanya kolabo na watu maarufu, nafanya na chipukizi na ni moja kati ya juhudi za kuwafanya waimbaji ambao wako chini dunia iweze kuwaona,” alisema.

Gozbert alizungumzia pia msimamo wa nyimbo za injili kwa sasa, wasanii au nyimbo anazozikubali na mengine mengi kuhusu kazi zake.

Angalia video ya mahojiano yote sehemu ya kwanza:

Bruno Mars afunika Grammy 2018, wanawake walia na usawa
Polepole aibua mapya shambulio la Lissu kupigwa risasi