Msanii wa muziki wa Injili, muandishi wa nyimbo na Staa wa ngoma ya ‘Ipo Siku’ kutoka Tanzania, Goodluck Gozbert sasa ameamua kuja na wimbo mpya unaoenda kwa jina la ‘Shukrani’ akiwakumbusha mashabiki zake kutoa shukrani kwa kila jema katika maisha wanayoyaishi.

Goodluck kupitia kibao chake kipya, ”Shukrani” mistari iliyopo kwenye kibao hiko ni shuhuda tosha juu ya maisha yake ambapo amezungumzia mambo mengi yanayogusa maisha yake.

Hata hivyo Goodluck mbali na uwezo wake katika uandishi na uimbaji, pia kwa taarifa sahihi na ya kuaminika ni kuwa anashiriki kwa asilimia kubwa katika kuandaa nyimbo zake mwenyewe kwa upande wa kucheza ala za muziki mwanzo wa kazi mpaka mwisho kama mtayarishaji mkuu wa kazi zake.

Neymar aruhusiwa kufanya mazungumzo na Paris St-Germain
Serikali yaongeza masaa ya mama kunyonyesha