Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuunda timu ya watu wenye uzoefu mkubwa na wanaoijua siasa ya madini kimataifa, ili kuweza kupata soko kubwa zaidi.

Ametoa ushauri huo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza mbele ya Rais Magufuli kwenye mkutano mkuu wa kisekta wa wizara ya madini.

Amesema kuwa ni vyema akaunda timu ya watu wenye ‘exposure’ kwenye siasa ya madini, kwani itasaidia kuweza kupenya kwenye soko la kimataifa.

“ Leo umekuwa kama Nabii, nitoe ushauri kwa Mh. Rais, si kweli kama hakuna soko la madini, dhahabu yenyewe ni fedha, isipokuwa nashauri kama ikikupendeza, uwe na watu wenye exposure kwenye siasa za madini kimataifa, sisi kwa asili tuna dhahabu, huwezi kutuambia tumechukua dhahabu ya wengine tuthibitishe ni za kwetu, hizo ni siasa tu za masoko, unaweza ukaunda watu wenye exposure ambao wanaweza kufikia masoko mbali mbali duniani”, amesema Askofu  Gwajima.

Aidha, Mchungaji Gwajima ameongeza kuwa madini tuliyonayo ni mengi na yanakosa soko kutokana na sababu mbali mbali, na iwapo yangelipiwa ushuru yasingezagaa, hivyo kama ambavyo aliwahi kukutana nayo watu wakiyauza kwenye bakuli barabarani.

Rais Magufuli amefanya Mkutano na wadau wa Sekta ya Madini, ambao pia uliwakutanisha na wadau na wafanyabiashara ya madini yaliyopo nchini.

Treni ya kifahari yaleta Watalii 61
Video: Walimu wabovu waziponza shule za Umma