Kila kizuri hakikosi kasoro, tunafahamu uwezo mkubwa alionao Diamond katika kuburudisha lakini pia tunafahamu uwezo mkubwa alionao Alikiba upande wa sauti ya kumtoa nyoka pangoni.

Ni dhahiri kuwa uachiwaji wa nyimbo za wasanii hawa nyota nchini unategemeana hasa upande wa You Tube ambapo viewers hushindanishwa.

Mfano mwaka jana Alikiba aliachia ngoma yake ya ‘Seduce Me’ hali iliyofanya Diamond apate kiwewe akaachia ngoma ya Zilipendwa akiwa amewashirikisha kundi la wasanii wake wote, ushindani ulikuwa mkubwa kwa muda mchache ngoma hizo zilitazamwa na mamilioni ya watu na kuzipaisha juu nyimbo hizo kuwa trendings kwenye YouTube channel Tanzania na nje ya nchi.

Kwa mara nyingine tena mara baada ya Alikiba akiwa amemshirikish kijana wake Cheedy na Ommy Dimpozi kuachia ngoma yao ya Rockstar, Diamond naye ameibuka na kuachia ngoma ambayo ameifanya peke yake baada ya vimaneno maneno vya chini kusambaa vikidai kuwa Diamond Platnumz anabebwa na kolabo anazofanya na wasanii wakubwa.

Ameachia goma yake inayoenda kwa jina la ‘The one’ ni wimbo uliopokelewa kwa namna tofauti tofauti na kitendo cha wawili hao kupishana siku mbili kuachia nyimbo zao kimewapigisha hatua kubwa sana katika kutambulisha nyimbo zao.

Nini maoni yako maana kuna wadau wanasema wasanii hawa wanaogoana, wewe unasemaje tazama video hapa chini tuandikie maoni yako.

Seneta amkalia kooni Trump, ataka ang'olewe madarakani
Maelfu ya wananchi waandamana Morocco

Comments

comments