Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amesema kuwa huwa anasimamia kile ambacho anakiamini na kwamba hawezi kuishi kinafiki.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akifanya mahojiano na kipindi cha 360 kinachorushwa na Luninga ya Cloudstv.

Amesema kuwa chama chake kinasimamia misingi imara na ya uwazi hivyo hawezi kuogopa kusema kile anachokiamini na kukisimamia katika maisha yake.

“Unajua chama chetu kinasimamia uwazi na ukweli hivyo, kimetulea kwenye hilo, hivyo binafsi siwezi kuishi kinafiki kwani maisha hayo ni magumu sana,”amesema Bashe

 

Majaliwa aanza kuwaneemesha wakulima wa pamba
China yaimarisha uhusiano na Tanzania, yatoa mamilioni

Comments

comments