Dar24 Media tayari tumeweka kambi kukuletea yanayojiri katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2019 na usiku huu maandalizi yanaendelea ambapo washiriki mbali mbali wameshawasili huku wafanyakazi wa kampuni ya DataVision International ambao wameshawasili pia kwa ajili ya kushiriki wametangaza kuibuka na ushindi na kunyakua medali nyingi katika mbio zote.

Kwa upande wa waandaaji wa mashindano hayo wameeleza namna walivyojipanga kuhakikisha kuwa mashindano yanafanyika na kumalizika vizuri kabisa huku wakiimarisha ulinzi, huduma mbali mbali za msingi kwa wakati wote wa mashindano.

Mashindano hayo yatafanyika kesho Machi 3, 2019 mkoani Kilimanjaro.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 3, 2019
Habari Picha: JPM aongoza maelfu ya wananchi jijini Dar es salaam kuaga mwili wa marehemu Ruge Mutahaba

Comments

comments