Kaimu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) na Mbunge wa Jimbo la Kaliua lililopo mkoani Tabora, Magdalena Sakaya amesema kuwa hali ya kisiasa nchini ni tete.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa kamata kamata inayoendelea kwasasa dhidi ya wanasiasa haijawahi kutokea katika historia ya Tanzania.

“Kwakweli kwa sasa hali ya kisiasa ni tete, wanasiasa wanakamatwa bila sababu za msingi, wakuu wa wilaya nao kila siku wanavurugana na kugombana na wanasiasa kitu ambacho hakijawahi tokea katika historia ya nchi hii,”amesema Sakaya

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 14, 2018
Dkt. Tulia adai hoja ya Peneza haikufuata utaratibu