Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amesema kuwa tatizo la uchafuzi wa mazingira hapa nchini ni kubwa  na linahitaji kuchukuliwa juhudi za makusudi ili kuinusuru nchi  kugeuka kuwa jangwa .
Makamba amesema  hayo leo Desemba 1, 2016 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na wahariri  ofisini kwake jijini Dar es salaam, Makamba amesema kutokana na ziara yake ya aliyotembelea  mikoa 10 hapa nchini ilikuwa na lengo la  kujionea hali ya mazingira na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji ambapo katika ziwa Rukwa limeathiliwa na wakulima.

 Aidha, Makamba amesema anakusudia kutangaza safu za milima ya mbeya kuwa eneo nyeti la uhifadhi mazingira na maeneo mengine nchini  yanayofanana na hayo na ameziagiza halmashauri zote nchini kuyawekea alama.
Hata hivyo, Makamba amewataka wahariri na waandishi wa habari kusaidia kutoa elimu kwa jamii juu ya kuhifadhi mazingira ikiwemo kupanda miti.
” Nimewaita leo kuwaomba  tusaidiane na kushirikiana kuifanya nchi yetu na jamii yetu na watu wetu watoe kipaumbele kwenye masuala ya hifadhi ya mazingira”  amesema Makamba.

Aliyetishia kumuua Trump mitandaoni aonja joto la jiwe
'Sh. bilioni 40 zimepelekwa Wizara ya Afya kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba' - Majaliwa