Hali imezidi kuwa tete katika baadhi ya maeneo jijini Dar es salaam mara baada ya mvua kubwa kuendelea kunyesha jijini humo.

Katika eneo la Jangwani ambalo limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara na kusababisha kufungwa kwa barabara, jana lilisababisha kusitishwa kwa usafiri wa mabasi yaendayo kwa haraka maarufu kama Mwendo kasi.

Wakizungumza na Dar24 Media wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa kero hiyo ya mafuriko imekuwa ni sugu kwa kila inaponyesha mvua mafuriko yamekuwa yakitokea.

 

Rais asema Taifa lakumbwa na msiba mkubwa
Mahakama Kuu yasitisha matumizi ya kanuni za mtandaoni