Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amelitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa weledi na kuepuka kuwabambikia kesi wananchi.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa atafanya ziara za kushtukiza ili kuweza kujionea utendaji kazi wa jeshi hilo ambao umekuwa ukilalamikiwa.

“Niwaambie tu kwamba hamjui saa wala siku ambayo Ninja ataingia, nimesikia kuna mambo mengi yanalalamikiwa, mimi nitafanya ziara za kushtukiza, na nawataka mkae mkao wa kula,”amesema Lugola

 

Video: Kifo cha mama angu kimechagizwa na mimi kufungwa Jela- Sugu
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 29, 2018