Harmonize maarufu kama Konde Gang, Jeshi la mtu mmoja tayari ameachia ngona yake ya Uno iliyosumbua katika kona mbalimbali za mitandao ya kijamii ikiwemo YouTube kwa kuwa namba moja ”Trending” siku moja mara baada ya kuachiwa sauti ya wimbo huyo na kukaa kileleni ikishikilia nafasi hiyo kwa takribani siku 7 sawa na wiki moja.

Ni ngoma iliyosubiriwa kwa hamu zote, kwani ni ngoma ambayo ilikuwa inapima uwezo wa Hormonize akiwa nje ya kundi alilojing’oa Wasafi na kuona kama bado anaweza kufanya maajabu, kwani msanii mwenza Rich Mavoko mara tu baada ya kujiondoa kundini, na nguvu yake ikafifia si Mavoko yule aliyekuwa ndani ya Wasafi bali Mavoko yule kabla ya kujiunga Wasafi.

Harmonize ameonekana kujipanga, Uno ni ngoma nzuri ameifikisha mbali na huenda ikamletea tuzo mbalimbali, tayari Harmonize ameonekana kukubalika na watu, kama tulivyoona tamasha aliloandaa Mbagala akiutambulisha wimbo huo wa Uno, watu walijitokeza kumshangilia na kumpa sapoti.

Tazama ngoma ya Uno hapa chini, kisha shusha komenti yako je ameitendea haki au amepuyanga?

Yanga yamfungashia virago Zahera mchana kweupe
CAG Kichere akabidhiwa ofisi na Assad "nitalinda kwa wivu", afunguka mahusiano na Bunge

Comments

comments