Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa amesema kuwa mgombea ubunge jimbo la Monduli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Julius Kalanga sio saizi yake.

Ameyasema hayo katika kampeni za kumnadi mgombea ubunge jimbo la Monduli wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Amesema kuwa mgombea wa Chama Cha Mmapinduzi CCM sio saizi yake hivyo anamwachia mwanae Fredy ili kuweza kupambana naye.

“Hata waje CCM miamoja hawaniwezi, tutawashinda mchana kweupee, halafu huyu mgombea wao sio saizi yangu, namuachia Fredy,”amesema Lowassa

JPM afanya uteuzi wa Kamishna wa TAKUKURU
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 6, 2018

Comments

comments