Mgombea wa kiti cha Ubunge Jimbo la Kinondoni kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu amesema kuwa wao hawashindani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) bali wanashindana na Dola.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa wao kama chama cha upinzani wamekuwa wakipambana na dola badala ya chama tawala CCM.

Amesema kuwa baadhi ya mawakala na wasimamizi wa vituo vya uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni ni makada wa CCM.

“Sisi hatushindani na CCM bali tunashindana na dola, wasimamizi wengi wa vituo vya uchaguzi ni makada wa chama tawala, hivyo kila kitu wanachokifanya ni kwa ajili ya kusaidia chama chao,”amesema Mwalim

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 18, 2018
Kitakacho wakuta CUF wasimlaumu mtu- Kamanda Mambosasa