Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo amesema hataki kusikia kuna mgao wa umeme na hategemei tena kuona kuna kukatika katika kwa nishati hiyo, aidha ameongeza kuwa ili kujenga nchi ya viwanda lazima kuwe na umeme wa uhakika, unaotabirika na nafuu.

Amesema hayo alipokuwa katika uzinduzi wa mradi wa uboreshaji wa huduma ya umeme leo Novemba 16,2016 jijini Dar es salaam, amesema kuwa Serikali inashirikiana na Serikali ya Finland kwenda kwenye madini ambayo ni ya kisasa kulinga na teknolojia inavyobadilika.

Mbarawa azindua bodi mpya TRL
Video: Majaliwa azindua mradi wa uboreshaji umeme Dar