Marehemu Doglas David ambaye alikuwa mwaandishi wa habari katika chombo cha habari cha  TBC, alifariki dunia akiwa chumbani kwake na mwili wake ulikaa ndani takribani siku zaidi ya nne hadi pale ulipoanza kutoa harufu ndipo majirani walipogundua na kuchukua hatua.

Ambapo Walifungua mlango na kukuta mwili ukiwa tayari umeharibika vibaya ndipo hatua za kuupeleka mwili hospitali ya Muhimbili zilichukua nafasi.

Hata hivyo Doglas hakuwa na ndugu jijini Dar es salaam jambo lililopelekea waandishi wa habari, marafiki wa karibu pamoja na wafanyakazi wenzake kulibeba suala hilo na kuhakikisha mwili wa Doglasi unapumzishwa salama katika nyumba yake ya milele mkoani Rukwa, Sumbawanga mjini ambapo wazazi wa Doglas waliomba mwili huo usafirishwe na uzikwe huko.

Tazama na sikiliza Video nzima hapa chini kufahamu historia fupi ya marehemu Doglas, Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali peme peponi.

Mkurugenzi mtendaji wa Dar Mpya amehadithia zaidi.

Waziri atangaza maeneo waliyotenga kutibu watakao pata virusi vya Corona
CCM Mara kumhoji Lugola

Comments

comments