Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Ally Mwalimu amesema kuna baadhi ya Halmashauri nchini zinaficha taarifa za wagonjwa wa Kipindupindu kwa kuhofia kutumbuliwa na Rais John Pombe Magufuli kwasababu alitangaza kuwachukulia hatua Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambao sehemu zao kutakuwa na njaa, Kipindupindu na Madawati.

Waziri Ummy amesema kitendo hicho cha kuficha wagonjwa wa Kipindupindu siyo tu suala la kukiuka maadili ila na sawa sawa na mauaji kwani baadhi ya hospitali wagonjwa hao wanachanganywa na wagonjwa wengine hali inayosababisha ugonjwa huo kusambaa zaidi.

Ummy amesema kutoa taarifa za Kipindupindu siyo suala la hiali kwani taarifa hizo zinasaidia hatua za kupambana na ugonjwa huo, Aidha amesema ni lazima Halmashauri na Mikoa kuhakikisha zanachukua tahadhari zote zinazohitajika kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huo.

 

Video: Waziri aitaja mikoa 10 kuhusu huduma za Saratani ya kizazi

Mzee wa miaka 75 aweka bango mtaani kusaka mke
Wananchi watakiwa kuhifadhi fedha zao benki