Hatimaye Hussein Machozi amerejea rasmi kwenye muziki kwa kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Nipe Sikuachi’.

Hussein amevunja ukimya wa muda mrefu uliotanguliwa na tangazo lake la kuachana na muziki na kujiendeleza kielimu nchini Italia.

Video ya wimbo huo imefanyika Gressoney-La-Trinity nchini Italia na imeongozwa na Alessandro. Audio ya wimbo huo imepikwa na Man Walter ndani ya studio za Combination Sounds.

Katika video hiyo, Hussein anamzimia mrembo ambaye bado yuko na mahabuba wake na anajaribu kumshawishi arejee kwake.

Inakuwa kama ajali baada ya mazoezi ya kuteleza kwenye barafu yanayomshinda Hussein na kumuangusha chini, ambapo mrembo huyo anakuwa mtu wa kwanza wa karibu wa kutoa msaada.

Msaada huo uligeuka kuwa kiunganishi kati ya wawili hao ukishuhudiwa na mbwa rafiki wa Machozi.

Enjoy simulizi zuri na video nzuri:

Whatsapp Yawavuruga Watumiaji Marekani, Ulaya
Wakandarasi wa ndani kunufaika na miradi isiyozidi thamani ya bilioni 10