Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Haki za Binadamu, LHRC, Dkt. Hellen Kijo-Bisimba amesema kuwa vitendo vinavyoendelea vya mauaji ya wanandoa ni vya kinyama.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa wanawake hawako salama ndio maana wamekuwa wakipambana na ukatili wa kijinsia.

Amesema kuwa wanawake wanapata shida sana kwa kupigwa majumbani, huku jamii ikichukuliwa vitendo hivyo ni vya kawaida kufanyiwa kwa mwanamke.

“Mimi siwezi kuelewa kwamba mtu akiwa na wivu wa mapenzi anatakiwa amuue mwenzie, nachojua ni kwamba mtu akiwa na wivu lazima ampende sana mwenzie,”amesema Dkt. Bisimba

 

Marcos Rojo: Hatutorudia makosa ya 2014
Mjue Mtanzania atakayecheza kombe la Dunia mwaka huu Urusi