Idadi ya wanaume wanaofanyiwa ukatili na wake zao imeongezeka baada ya kutolewa kwa elimu kuhusu masuala ya jinsia.

Hayo yamesemwa na Anna Henga Mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) alipokuwa akizungumza na Dar24 Media.

Amesema kuwa idadi ya wanaume wanaojitokeza kuomba msaada wa kisheria kuhusu manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa wake zao imeongezeka ikilinganishwa na hapo awali.

“Kwa sasa muamko ni mkubwa sana kwa wanaume tofauti na hapo awali, wanajitokeza wengi sana kuomba msaada wa kisheria kuhusu manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa wake zao,”amesema Henga

Hata hivyo, ameongeza kuwa ukatili wa kijinsia umeongezeka ikilinganishwa na miaka iliyopita, ambapo unatokana na mabadiliko ya maisha.

Zitto aomba kampeni za Ubunge Kinondoni, Siha kusitishwa
Wafanyakazi wakatwa mishahara kuchangia uchaguzi