Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amepokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni 120 kutoka kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa.

IGP Sirro amepokea hundi hiyo kwa ajili timu ya jeshi la polisi Tanzania pamoja na vifaa vya michezo vyenye thamani ya mamilioni, ambapo makabidhiano hayo yamefanyika leo Septemba 11, 2017 makao makuu ya Jeshi la Polisi, Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Jeshi hilo pamoja na SportPesa iliyowakilishwa na Abbas Tarimba.

Magazeti ya Tanzania leo Septemba 12, 2017
Video: Majaliwa aguswa na Masenga, ampa msaada wa milioni 10