Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewatoa hofu wazazi wa watoto kuhusu utekwaji wa watoto uliokuwa ukifanywa na baadhi ya kikundi cha kihalifu huku akisema kuwa kwa sasa mabo yanaenda vizuri.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kwa sasa wameweza kuwadhibiti wahalifu hao na kwamba bao wanaendelea na kuushughulikia mtandao huo.

Aidha, katika hatua nyingine, IGP Sirro amezungumzia suala la kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuwa watapatikana ikiwa wananchi watasaidia jeshi hilo kupata taarifa za wahalifu hao

Amesema kuwa usalama wa nchi upo vizuri na kuwa mpaka sasa jeshi la polisi limeongeza nguvu ya upelelezi mjini Dodoma ili kuhakikisha linawapata watu ambao wamefanya uhalifu wa kumpiga risasi mbunge huyo, huku akiwataka wananchi wasihusishe tukio hilo na masuala ya kisiasa.

“Naomba wananchi wasidanganywe kwenye suala zima la siasa na vitu vingine hapa huwa nasema siku zote kama hakuna amani na usalama, siasa haiwezi kupata nafasi ili tukio limetokea tunapeleleza na tupo makini na hili tukio, kwa sasa tumeongeza vikosi vya upelelezi Dodoma, wale waliofanya lile tukio ni lazima tutawakamata ila upelelezi huu unaweza kuzaa matunda mazuri zaidi endapo wananchi watatupa ushirikiano wa kutosha,”amesema IGP Sirro

Lissu atolewa chumba cha upasuaji
Video: Jisalimisheni wenyewe kabla hatujaanza kuwakama- IGP Sirro