Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman ameuelezea Mpango Mkakati wa Mahakama kwa Miaka Mitano pamoja na Mradi wa Maboresho ambao utazinduliwa rasmi Septemba 21, 2016 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.

Jaji Chande amesema hayo leo Septemba 19, 2016 wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema mpango huo wa Mahakama kwa miaka 5 ndiyo utakuwa dira na mwelekeo wa Mahakama ya Tanzania.

Mpango huo upo tayari na umeanza kwa Mahakama ya Tanzania kushirikiana na wadau mbali mbali wa nje na wandani wa Mahakama kwa kuanza kufanya tathmini juu ya hali ya Mahakama na kazi zake za msingi kuhusu utoaji haki kwa mashauri yanayofikishwa Mahakamani.

jaji Chande pia amesema kuwa mpango huo wa Mahakama una nguzo kuu tatu, matokeo makubwa nane na malengo 17.  Bofya hapa kutazama video.

Matonya na vijana wake wamlilia Magufuli
Japan kukarabati shule zilizoharibiwa na tetemeko Kagera