Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma, amerudia kusisitiza nia ya Serikali kuhamia  Dodoma katika kipindi chake cha uongozi ili kutekeleza ndoto ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kutaka makao makuu ya nchi yawe Dodoma.

Pia Rais Magufuli amesisitiza wananchi na wanasiasa kutunza amani na kudumisha amani iliyokuwepo nchini. Pia amewataka Watanzania wote kuendelea kuwaenzi mashujaa walioipigania nchi hii.

Mzee wa Upako: Lowassa ni tishio CCM
JB Afunguka Kuhusu Bongo Movie Wanaokimbilia Kwenye Muziki.