Hatimaye wimbo maalumu wa kombe la Dunia umetoka ambapo msanii maarufu Marekani Jason Derule ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya ”Tip Toe” ameachia ngoma hiyo ya ‘Colours’ aliyomshirikisha msanii mkubwa wa Bongo Fleva Tanzania, Diamond Platnumz.

Wimbo huo utatumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2018 inayotarajiwa kufanyika nchini Urusi, kama ambavyo wimbo wa Wakawaka ulioimbwa na Shakira na kutumika katika michuano ya Kombe la dunia mwaka 2010.

Wimbo wa ‘Colours’ umedhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola.

Mapema leo hii katika ukurasa wa Instagram ya Diamond Platinumz amepost video ya Jason Darulo akiwakaribisha watanzania na dunia kwa ujumla kuusikiliza wimbo huo alioimba na Diamond Platinumz.

Bonyeza kitufe hapo chini chenye alama ya ‘Play’ kusikiliza wimbo hupo

Kenyatta apangua hoja inayohusu masuala ya ushoga
Bashar Al- Assad aikataa tuzo kutoka Ufaransa

Comments

comments