Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewakamata wachina wawili waliokuwa wamemteka mfanyakazi wa hoteli ya Palm Beach iliyopo Jijini Dar es salaam, ambapo watekaji hao walikuwa wanahitaji fedha za kichina, YUAN 100,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 32.2 za kitanzania.
Akiongea na waandishi wa habari Oktoba 26, 2016, Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro amemtaja raia huyo kutoka China aliyekuwa ametekwa kuwa ni Liu D/O Hong ambapo watekaji hao ambao hadi sasa wanaoshikiliwa na jeshi la Polisi wamefahamika kwa majina ya Wang Young Jin na Cheng Chung Bao wote wakiwa ni raia kutoka China.
Kamanda Sirro amesema kuwa kikosi cha kupambana na wezi wa magari cha polisi, Kanda maalum Dar es salaam kimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa makosa ya wizi wa magari, watuhumiwa hao ni pamoja na Denis Gasper Ushaki mkazi wa Manzese Uzuri, Alfred Ditriki mkazi wa Sinza, Venance Avity Bureta mkazi wa Mbezi na Valentino Godfrey mwanafunzi wa Chuo cha CBE.
Kamanda Sirro ameongeza kuwa jeshi la polisi limefanya operesheni mbalimbali ndani na pembezoni mwa Jiji la Dar es salaam na kufanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 57 kutoka sehemu za Gongo la mboto, Tandika, Ukonga, Kunduchi, Kawe na Keko, watuhumiwa hao wamekamatwa kwa makosa mbalimbali kama vile, kuvuta na kuuza Bangi, Uuzaji na unywaji Gongo.
Aidha, Kamanda Sirro amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Usalama barabarani limekusanya jumla ya shilingi milioni 690,120,000 katika kipindi cha siku saba
Video: Alichosema Kamanda Sirro kuhusu dada aliyesambaza taarifa ya uhalifu