Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limesema katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka 2016 watu wengi hupenda kusafiri kwenda maeneo mbalimbali na hivyo kuongeza matumizi ya vyombo vya moto barabarani, hivyo Jeshi la Polisi limejipanga vizuri ili kuwatia mbaroni madereva wote watakaokiuka Sheria za Usalama Barabarani na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa Sheria.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed R. Mpinga leo Desemba 22, 2016 wakati akiongea na waandishi wa habari, ambopo ameeleza kuwa wamejipanga ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa kushtukiza barabarani kwa kuwapima madereva ulevi na kuwakamata madereva wanaopita magari mengine yaliyoko mbele yao bila  kuchukua tahadhari.

Aidha , Kamanda Mpinga amesema katika Operesheni kali inayoendelea katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka  kuelekea mwanzoni mwa mwaka mpya, katika mikoa ya Geita, Kagera, Mara, Tabora, Lindi, Iringa, Shinyanga, Arusha, Kilimanjaro, Rukwa na Njombe takribani madereva 227 wamefikishwa Mahakamani wakitokea mahabusu.

Mpinga amesema pia wamelipa faini ta shilingi laki tatu (3) hadi shilingi laki sita (6) na wengine kifungo cha muda

Video: Kamanda Mpinga asitisha utendaji wa CHAKUA mikoani
Tanzania Yapanda Viwango Vya Ubora Wa Soka