Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limesema linaendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika kuelekea kusherekea sikukuu ya Eid El Fitri ili wananchi washerekee sikukuu hiyo kwa amani na utulivu na kupiga marufuku kufanyika kwa disko toto.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema Jeshi la polisi limeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha vitendo vya kihalifu vinadhibitiwa huku akiwataka wananchi kutofanya vitendo vyovyote vitakavyoashiria uvunjifu wa amani.

Juu ya suala la usalama barabarani kamanda Mambosasa amesema jeshi la polisi kupitia kikosi chake cha usalama barabarani kinaendelea na opereshani ya kamatakamata ya makosa yanayofanywa na watu wasiotaka kufuata sheria.

Katika hatua nyingine Mambosasa amesema mnamo Juni 5, 2018 majira ya saa nne usiku maeneo ya kitunda relini jeshi la polisi lilifanikiwa kukamata silaha aina ya bastola ya revova yenye namba ya usajili B86560 ikiwa haina risasi.

Pato la Taifa lazidi kuongezeka
Jamii Forums yawatahadharisha wateja wake

Comments

comments