Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Muliro Jumanne Muliro amesema kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri kuhakikisha siku ya uchaguzi panakuwepo na hali ya usalama.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewataka wananchi wa Jimbo la Kinondoni kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura.

Amesema kuwa jeshi hilo limejipanga kikamilifu kuhakikisha hali ya usalama inakuwepo muda wote, hivyo amewataka wananchi kuondokana na hofu.

“Tumejipanga vizuri kukabiliana na mtu yeyote atakayetaka kuhatarisha hali ya amani, tumeandaa dhana zote za kukabiliana na wale watakao taka kuleta uvunjifu wa amani, tutawashughulikia kikamilifu, hivyo wananchi msiwe na hofu yeyote pindi mtakapoona askari wengi,”amesema Kamanda Muliro

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 15, 2018
Video: Kauli 'tata' zamuweka matatani Mbowe, sasa kuchunguzwa

Comments

comments