Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan (JICA), Hiroshi Kato na kujadiliana mambo kadhaa yakiwemo ya nishati na miundombinu.

Katika mazungumzo hayo, Bw. Kato alimweleza Waziri Mkuu nia ya shirika hilo kuendelea kusaidia miradi mbalimbali ya kilimo hapa nchini na hasa katika sekta za afya, maji, kilimo na miundombinu ambazo imekuwa ikijihusisha nazo kwa muda mrefu sasa. Bofya hapa kutazama video #USIPITWE

Picha: Majaliwa ashiriki mkutano wa APRM- Nairobi
Majaliwa amwakilisha Rais Magufuli mkutano wa Wakuu wa Nchi TICAD