Kiongozi na mwakilishi wa Dar24, Christopher Kika kwenye uzinduzi wa kampeni ya Tupo Pamoja amefanunua zaidi kuhusu ujio wa kampeni hiyo na kueleza kuwa kampeni hiyo imezinduliwa rasmi kwa lengo la kusaidia watoto wote wenye umri chini ya miaka18 wenye matatizo mbalimbali ya kiafya.

Amesema kwa kampeni iyo imeanza rasmi kwa kuokoa maisha ya binti  Mariam anayesumbuliwa na ugonjwa wa tumbo (Intestinal Obstruction). Kampeni hiyo ni fursa kwa watoto wengine wenye matatizo ya kiafya kufarijika na kupata msaada wa kutatuliwa matatizo yao kiafya.

Aidha, ameeleza kuwa kupitia kipindi chao cha Mkasa kinachorushwa kipitia chaneli yao ya You tube (Dar24 Media), kipindi hiko kimelenga  kuiletea jamii simulizi mbalimbali za maisha ambazo watu wamepitia ikiwa ni lengo la kuelimisha jamii kupitia Mikasa hiyo.

Hivyo, Dar24 Media kwa udhamini mkubwa wa DataVision inafanya harambee kwa wananchi na wadau kwa ujumla kuchangisha pesa ya kitanzania Shilingi milioni 44 kwa ajili ya matibabu yake huko nhini India.

Hivyo amewaomba wananchi kumchangia Mariam kupitia Mlipa kwa Tigo Pesa Mpesa au Airtell Money, kwa kuandika kumbukumbu namba 400700 na namba ya kampuni 400700 lakini pia wamefungua akaunti ya benki ya CRDB kwa lengo la kumchangia Mariam kupitia akaunti namba 0150021209500 jina la akaunti ni Data Vision International – Tuko Pamoja.


Video: Dar24 yazindua rasmi kampeni ya TUKO PAMOJA kumsaidia mtoto aliyefanyiwa oparesheni 10 bila nafuu

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 24, 2017
Safari za usiku zapigwa marufuku