Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa kama mmiliki wa Gazeti la Mawio lililofungiwa na Serikali kutoa habari zake anaona hajatendewa haki basi aende mahakamani.

Mwakyembe ameyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari wa kituo kimoja cha redio kilichopo jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa kama mmiliki huyo anaona hajatendewa haki basi anaweza kwenda mahakamani ili kuweza kupata haki yake ya anayohitaji.

“Unajua Kubenea anauswahili mwingi sana usiokuwa na maana yeyote, ukiangalia anawaandama viongozi wastaafu waliotangulia kwa tuhuma zisizokuwa na uhalali wowote, huku rais mstaafu aliyepita ndiye aliyemsaidia hata kumpeleka Indvia kwaajili ya matibabu,”amesema Dkt. Mwakyembe.

Hata hivyo, wiki iliyopita Serikali ililifungia gazeti la Mawio kwa muda wa miaka miwili kutojihusisha na uchapishaji wa habari za aina yeyote huku mmilki wa Gazeti hilo, Saed Kubenea akiibuka na kulalamika kuwa hajatendewa haki.

Wananchi watahadharishwa kuhusu ugonjwa wa Nguruwe
Urusi yaikung'uta New Zealand goli 2-0