Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wameongoza Maelfu ya Watanzania katika kuaga Mwili wa aliyekuwa Mtangazaji wa kituo cha Clouds FM Marehemu, Ephraim Kibonde nyumbani kwa Baba yake Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.

Katika ibada hiyo ya kutoa heshima za mwisho viongozi wengine wa kiserikali waliohudhuria ni pamoja na Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya yaKinondoni Daniel Chongolo.

Viongozi wengine waliofika katika Msiba huo ni pamoja na Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Suleiman Jaffo Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.

Aidha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini kwa umoja wao waliweza kufika katika msiba huo na kutoa faraja kwa wafiwa ambapo safari ya kuelekea Makaburi ya kinondoni kumpumzisha mpendwa  wetu Ephrahim Kibonde.

Timua timua yarudi tena Chadema, wawili wamwaga
Polisi wamtwanga mashtaka 16 muigizaji wa ‘Empire’