Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli Septemba 26, 2016 amefanya ziara bandari ya Dar es salaam na kuzungumza na wafanyakazi wa bandari hiyo ambapo ametoa miezi miwili kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kununua mashine nne za kukagulia mizigo bandarini hapo (Scanning Mashine).

Ametoa agizo hilo mara baada ya kubaini kuwa mashine nne za ukaguzi wa mizigo zilizopo ni mbili pekee zinzofanya kazi na hazina uwezo wa kukagua mizigo yote inayotoka na kuingia nchini katika bandari hiyo hali inayosababisha kutokuwepo kwa udhibiti wa uhakika wa udanganyifu.

”Nawaagiza TPA, na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Prof.Mbarawa na mamlaka ya mapato, hakikisheni mna nunua mashine za kukagulia mizigo nne ndani ya miezi miwili na ikifika miezi mitano muwe mmenunua mashine sita,ni lazima mizigo yote lazima ikaguliwe kwa mashine” – Rais Magufuli.

Aidha Rais magufuli ametembelea pia eneo la mita za kupimia mafuta yanayopakuliwa nchini (Flow Meters) na kubaini kuwa mita hizo hazifanyi kazi na kuiagiza( TPA) kuharakisha mchakato wa  kununua mita mpya na kuzifunga eneo hilo ili kudhibiti ukusanyaji wa kodi ya mafuta. Tazama hapa video

Sam Allardyce Ajivisha Kitanzi, Huenda Akapoteza Kazi
Aubameyang Akoleza Moto Wa Usajili