Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amekabidhi milioni hamsini kwa viongozi wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) mara baada ya kuwaalika wachezaji wa timu ya taifa (Taifa Stars) Ikulu jijini Dar es salaam na kutahadharishi kuhusu matumizi ya fedha hizo.

Katika hafla hiyo Rais amewataka wachezaji kujituma zaidi huku akiwaeleza wazi kuwa hajafurahishwa na matokeo ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Cape Verde hapa nyumbani kwani bado tunadaiwa bao 1 baada ya kufungwa mabao 3-0 ugenini.

”Nawakabidhi shilingi milioni 50, nahodha wa Taifa Stars na Rais wa TFF mbele ya Waziri Mwakyembe hapa hapa muondoke nazo lakini mkashinde na zitumike vizuri kwa ajili ya wachezaji, msiposhinda niwaambie kabisa mtazitapika kwa namna nyingine”, amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais amewataka Rais wa TFF, Wallace Karia na Waziri mwenye dhamana ya michezo Harrison Mwakyembe kuhakikisha timu hiyo inafuzu AFCON 2019 kwa kushinda mechi mbili zilizobaki dhidi ya Uganda na Lesotho.

Hata hivyo, Taifa Stars ambayo ipo kundi L na timu za Uganda, Cape Verde na Lesotho, ina alama 5 katika nafasi ya pili nyuma ya Uganda yenye alama 10 kileleni.

 

Mwanafunzi ajifungua kwenye choo cha shule
Hatua 5 za Kuchukua Mfanyakazi Mwenza Akijisifia Kwa Kazi Yako