Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameagiza wote wanaohusika na MV Nyerere wakamatwe na watakaobainika kuhusika kwa uzembe wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi wakati akitoa tamko rasmi la Serikali kuhusu ajali ya MV Nyerere ambapo Rais ameagiza pia bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia kesho Septemba 22, 2018.

“Serikali inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa ndugu waliofarii katika ajali ya MV Nyerere na kuwatakia majeruhi wapone haraka,”mesema Balozi Kijazi

Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama jana mchana Septemba 20, 2018 imefikia 137 huku uokoaji ukiendelea.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Issack Kamwelwe amesema miili 37 tayari imetambuliwa na ndugu na jamaa wakati kazi ya kuitambua iliyosalia ikiendelea.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 22, 2018
Video: Mbowe ameomba 'poo' akajipange upya hajasusia chaguzi - Polepole