Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli leo kwenye ziara yake Mkoani Mwanza akihutubia katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa meli ya MV.Butiama na MV. Victoria amewapongeza wabunge wa CCM kwa kupitisha bajeti ya serikali na kuwananga wabunge kutoka vyama vya upinzani kwa kupiga kura ya hapana kwenye kuipitisha bajeti hiyo.

Magufuli amesema iwapo wabunge wa CCM wangepiga kura ya hapana kama wabunge wa upinzani serikali isingeweza kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemu wa ujenzi wa meli mpya unaotarajia kuanza hivi karibuni.

Amesema kuwa kura ya hapana maana yake watu wa Bukoba waendelee kupata tabu, watu wa Victoria wasiweze kufanya biashara na waendelee kuteseka kwa  kukosa usafiri ndani ya Ziwa Victoria.

Aidha, Rais Magufuli amewapongeza wabunge wa CCM kwa kuwawakilisha vyema wananchi wa Bukoba na amawaomba waendelee hivyo hivyo.

Tazama hapa, Rais Magufuli akizungumza hayo.

Serikali yajipa siku 14 kulipa bilioni 3.7 limbikizo la mishahara ya miezi 27
China kutoa dola bilioni 60 kusaidia Bara la Afrika