Baada ya kuhakikishiwa kuwa kuna amani na usalama nchini Burundi na Rais wa nchi hiyo, Piere Nkurunzinza, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewataka wanachi wenye asili ya Burundi waliopo nchini Tanzania wafanye wawezavyo kwa hiari yao warudi kwao wakaijenge nchi wasisingizie kuna vita.

Ameyasema hayo mapema hii leo wakati akihutubia wakazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera katika mkutano wa hadhara uliyofanyika katika viwanja vya Posta baada ya kupokea ugeni kutoka nchini Burundi wa rais huyo pamoja na baraza lake la mawaziri kwa mazungumzo ya kiuchumi.

“Ndugu zangu warundi mmesikia taarifa iliyotolewa na Rais Nkurunziza anawaomba mrudi kwenye nchi yenu, mkajenge nchi yenu, mkajitafutie maisha, ni kama wanaotoka Afrika kwenda Itali lakini kuna wakimbizi wamezoea kukimbia tu, sasa kwa sababu Rais ameshawaambia mrudi nyumbani sasa mchukue hatua za kurudi nyumbani kwa hiyari wala sisi hatuwafukuzi. Ninafahamu wapo baadhi ya watu ambao hufanya biashara na wakimbizi kwa sababu ndipo wanaotoa vyakula,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Aidha, amesema kuwa kuwa kuna baadhi ya wakimbizi ambao wameahidiwa kupewa shilingi elfu kumi kumi ili wabaki lakini amewataka warudi ili wakapewe hizo fedha wakiwa nchini mwao kwakuwa ameshazungumza na Rais wao kuwa kuna amani na usalama.

Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli ameunga mkono ombi la Rais wa Burundi alivyowataka wananchi wake warudi kwao wakaijenge kwa pamoja nchi hiyo kwa kuwa hakuna shida ya aina yoyote katika kipindi hiki.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amemthibitishia Rais Nkurunziza kuwa Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa majirani zake wote waliopo ndani ya Afrika Mashariki ndani ya SADC pamoja na nchi ya Burundi.

Video: Jeshi la Polisi Dar lawataka wahalifu kujisalimisha
Video: TCU yatii agizo la JPM, yatangaza rasmi taratibu za kujiunga na vyuo vikuu