Mkuu wa Wilaya ya Arumeru iliyopo mkoani Arusha, Jerry Muro amemsweka ndani mwananchi mmoja wilayani humo mara baada ya kutoa majibu ambayo hayakumfurahisha DC Muro akisema kuwa kilichofanywa na mtu huyo kinaashilia dharau.

DC Muro amefikia uamuzi huo alipokuwa akizungumza na wananchi wilayani humo kuhusu mgogoro wa ardhi ambao umedumu kwa muda mrefu.

Amesema kuwa ni bora wananchi wa wilaya hiyo iliyopo mkoani Arusha waruhusu wataalam wa ardhi kupima ili kuweza kuondokana na migogoro isiyokuwa na tija.

“Kama mmeshindwa kufuata sheria za nchi, ondokeni mkatafute sehemu nyingine za kuishi, mimi kama msimamizi na kiongozi hawezi mtu kunijibu kama huyu, hii ni dharau,”amesema DC Muro

Video: Hawa ndiyo marais wenye ulinzi mkubwa zaidi duniani
Serikali yajipa siku 14 kulipa bilioni 3.7 limbikizo la mishahara ya miezi 27

Comments

comments