Staa wa Bongo Movie, Jacob Steven maarufu kama JB amesema kuwa msanii yoyote wa filamu nchini anayeishi kwa kutegemea uigizaji lazima azungumzie yale yanayokwamisha maendeleo ya ukuaji filamu na maendeleo kwa waigizaji wenyewe.

Amesema yeye mwenyewe anategemea filamu tu hivyo hawezi kukaa kimya lazima apige kelele kwani hayupo kisiasa na atashirikiana na upande wowote wenye nia ya kusaidia tasnia ya filamu nchini, kwani nia yao si kutaka movie za nje ziondolewe bali wanaofanya biashara ya movie za nje walipie sawa sawa na wanavyolipia wasanii wa ndani.

JB amesema hayo katika uzinduzi wa filamu yake mpya ya ‘Kumekucha Tunu‘ ambayo ina maudhui makubwa ya kilimo kwa lengo la kupeleka ujumbe kwa jamii juu ya faida za kulima na namna ambavyo kilimo kinaweza kumuinua mtu mwenye kipato cha chini kabisa na kubadilisha maisha yake.

Amesema filamu hiyo ni tofauti na hizi za Bongo movie kutokana kwanza na bajeti yake kuwa kubwa na imeongozwa na muongozaji mkubwa, hivyo inaweza kuonyeshwa sehemu yoyote duniani.

Makamba atoa neno kuelekea Maadhimisho ya Muungano
Video: Kendrick Lamar na Eminem ‘Washindanishwa’, Mijadala Yateka Vituo