Kamanda wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga ametangaza kusitisha utendaji wa Chama cha Kutetea Abiria (CHAKUA) mikoani kwani utendaji wao umekuwa mbaya, kukiuka maadili na kujikita katika usimamizi wa sheria badala ya utoaji wa elimu.

Kamanda Mpinga amesema hayo leo Desemba 22, 2016 wakati akiongea na waandishi wa habari, amesema kuwa Chama hicho kilikuwa kikishirikiana vizuri na Jeshi la Polisi pamoja na Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA) katika utoaji wa elimu hasa katika Kampeni ya Abiria Paza Sauti lakini kimekiuka maadili na kupelekea matatizo mbali mbali katiki vituo vya mabasi.

Amesema Chama hicho kimesitishwa mikoani kuanzaia sasa hasa katika vituo vikuu vya mabasi badala yake kitabaki katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo (UBT) tu.

Hata hivyo, Kamanda Mpinga amesema kuwa CHAKUA kitaruhusiwa kutoa Elimu katika vituo vya mabasi mikoani kwa idhini ya Makamanda wa Polisi wa mikoa (RPCs) wajihusishe na utoaji wa elimu tu, wasijihusishe na usimamizi wa sheria suala ambalo ni jukumu la Jeshi la Polisi.

Rais Magufuli amteua Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Video: Jeshi la Polisi kufanya ukaguzi wa kushtukiza barabarani