Kufutia taarifa za tukio la mtu mmoja kutekwa na kisha kutolewa macho na mtandao wa vibaka jijini Dar es Salaam, Jeshi la Polisi mkoani humo limeeleza  jinsi lilivyouzima mtandao huo.

Akiongea jana katika kikao maalum na wananchi wa Buguruni kilichohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Simon Sirro alisema kuwa hakuna mhalifu atakayesalimika baada ya kuwadhuru wananchi na mali zao.

Alisema Jeshi hilo lilimnasa kibaka huyo mtoa macho anayejiita scorpion na amefikishwa Mahakamani baada ya kutaja mtandao wake.

Kamanda Sirro pia aliwapa ujumbe mzito wakazi wa Buguruni kuhusu watoto wao wanaojihusisha na uhalifu huku akuwasogelea kwa msisitizo.

Angalia video hii kupata ujumbe mzito na onyo kali la Kamanda Sirro:

JPM amteua Prof. Lawrence Museru kuwa Mkurugenzi Mtendaji Muhimbili
Luis Enrique: Nipo Tayari Kulaumiwa Na Yoyote