Kamanda wa kanda Maalumu ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro leo Septemba 5, 2016 ametoa taarifa kuhusu Operesheni ya kupambana na majambazi iliyofanyika wiki mbili zilizopita na kufanikisha kukamata mtandao wa majambazi sugu watatu. Ambapo Operesheni hiyo ni kufuatia matukio ya kushambuliwa na kufariki Askari wanne na ofisa mmoja wa polisi kwenye matukio mawili ya kukabiliana na majambazi likiwemo lile la Vikindu Mkuranga mkoani Pwani na tukio jingine la ujambazi lililofanyika Mbande Dar es salaam.

Kamanda Sirro akiongea na waandishi wa habari, ameeleza kukamatwa kwa majambazi watatu ambao wamepatikana na silaha 23, risasi 835,  bullet proof 03, sare za polisi, Pingu 48, radio call 12 na vifaa vingine vingi vya kijeshi. Bofya hapa kutazama video

Video: Waziri Makamba Apokea Kamati Ya Mazingira Kutoka Sweden
Aishi Manula: Ninashukuru Kwa Pongezi Za Nyota Wa Nigeria