Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere amesema kuwa siku si nyingi mamlaka hiyo itaanza kuyafanyia kazi malalamiko na kero zilizotolewa na wachimbaji wadogo wadogo wa madini.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini uliofanyika kwa siku mbili.

Amesema kuwa wamepokea malalamiko hayo ambayo yamejikita zaidi katika utitiri wa kodi ambazo zimeonekana kuwakera wachimbaji hao, hivyo kuomba kuwepo mfumo maalumu ambao utaweza kupunguza usumbufu.

“Ni kweli kabisa wachimbaji wadogo wadogo wa madini wamelalamikia suala zima la utitiri wa kodi, hivyo sisi kama mamlaka husika tutashirikiana na wizara ya fedha pamoja na wizara ya madini ili kuweza kuweka mfumo mzuri wa ulipaji kodi,”amesema Kichere

Ujangili na Mauaji ya Tembo yapungua Nchini
Rais Magufuli aombwa kufuta leseni za kibiashara vyombo vya habari vya dini