Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema kuwa vyombo vya dola vitandelea kuimarisha amani na utulivu wa Tanzania ili kuhakikisha shughuli za maendeleo zinazoendelea hivi sasa kukamilika bila bughuza.

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akitoa hoja kuhusiana na taarifa ya makadirio ya bajeti kwa wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020, ambapo amesema atahakikisha amani inalindwa.

“Wizara itaendelea kulinda amani na usalama wa nchi hii kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola na wadau wengine, kuwepo kwa utulivu ambao watanzania wanauona utaendelea kuwezeshwa na hakika shughuli za maendeleo zitaendelea kuimarika,” amesema Lugola

Aidha, kuhusiana na zoezi la usajili wa laini kupitia vitambulisho vya taifa, Lugola amesema kuwa Watanzania milioni 16 ambao wana namba za vitambulisho vya NIDA wana sifa za kusajili kadi za simu ya mkononi, na Serikali inaendelea na utaratibu wa kutoa vitambulisho vya taifa kwa ambao bado hawajapata vitambulisho hivyo.

Wananchi waiangukia serikali kutokana na ubovu wa barabara
Video: Serikali yatoa ufafanuzi kuhusu umiliki wa Laini za simu

Comments

comments