Serikali imewataka Wananchi kuzingatia suala zima la kwa kuzibua mitaro ya maji yaliyopo katika mito ili kuepukana na adha ya mafuriko inayosababishwa na kuwepo kwa taka ngumu zinazozuia utiririkaji wa maji kwa urahisi.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Kangi Lugola katika uzinduzi wa Operesheni ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira ili kuweza kulisalimisha jiji la Dar es salaam itakayoanza tarehe 1 Novemba hadi Desemba 30 mwaka huu.

“Uzalishaji wa taka ngumu ambao tumekuwa tukiufanya umesababisha kuziba mifereji ya maji, mitaro, na mito matokeo yake maji yametafuta mahali pakupita yakakosa na kuvamia makazi ya watu na ndiyo maana ya mafuriko,” amesema Lugola.

Aidha, Lugola ametoa wito kwa wananchi kupitia Viongozi wa ngazi za mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya kazi ya kuwaelimisha wananchi na kutoa vitendea kazi ikiwemo magari ya kuzolea taka.

Hata hivyo, Lugola ametoa onyo kwa watendaji wa halmashauri watakaokwepa kushiriki katika operesheni hiyo na kuwaasa kutoa msaada wa hali na mali utaohitaji kutoka kwa wananchi ili kuhakikisha kuwa inabaki Tanzania salama

Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 31, 2017
Serikali yamjibu Zitto kuhusu Takwimu