Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kuwaruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu wafanye siasa vyuoni kwa taratibu zilizowekwa kwa sababu vyuo ni kitovu cha mabadiliko ya jamii ikiwa ni pamoja na kuwa chimbuko la viongozi mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu ambapo amekinzana na kauli ya Rais  Magufuli aliyoitoa siku chache alipotembelea Chuo cha Kilimo cha Sokoine kuwataka wanafunzi wasifanye siasa vyuoni.

“Kupiga marufuku siasa vyuoni ni kujenga taifa la vijana waoga, wasiokuwa na uwezo wa kuhoji.  Vijana msiache kuhoji mambo ya msingi kwa jamii zenu, hiyo ndiyo maana ya usomi,”amesema Shaibu

Hata hivyo, Chama hicho kimeshauri kuwepo kwa mfumo mpya wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, kutokana na mfumo uliopo sasa kutokidhi mahitaji ya wanafunzi hali inayopelekea wengi wao kukosa mikopo.

 

Utaitambuaje ngozi yako kuwa ni kavu? soma hapa
Video: Dkt. Slaa ajitosa sakata la Sh1.5 trilioni, Askari Polisi atekwa na wasiojulikana