Rapa anayetajwa na kukubalika kama mkali zaidi wa wakati huu, Kendrick Lamar ameachia video ya ngoma yake ‘DNA’, ikiwa ni moja ya pishi kutoka kwenye albam yake ya DAMN, saa chache zilizopita.

Video hiyo iliyoongozwa na Nabil pamoja na Little Homies imembeba muigizaji maarufu, Don Cheadle ambaye anaonekana kumfanyia mahojiano ya kiusalama Kendrick Lamar kuhusu DNA, lakini anajikuta yeye binafsi akiimba wimbo huo mbele ya mtuhumiwa wake( Kendrick Lamar).

DNA inatafsiriwa kama Dead Nig** Assassination.

DAMN ni albam ya rapa huyo ya kwanza kutoka studio tangu alipoachia albam ya mwisho ‘To Pimp a Butterfly’ mwaka 2015. DAMN  ni albam ya nne rasmi kutoka studio inayoonesha uwezo wa Kendrick ambaye awali alikuwa akiitwa K-Dot.

Mwaka jana, aliachia mkusanyiko wa nyimbo pamoja na demo kadhaa kutoka studio kwa ajili ya mashabiki wake.

Fahamu Katuni Zinavyoweza Kutafuna Ubongo wa Mtoto Wako na Kumpa ‘Kifafa’
Video: Majaliwa atoa agizo NEEC, Ataka ripoti kabla mwezi Mei, 2018