Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amesema kuwa afya ya mama yake Desderia Rungu Mbilinyi ilibadilika ghafla baada ya yeye kuhukumiwa kwenda jela.

Ameyasema hayo wakati akisoma wasifu wa mama yake kwenye ibaada ya kumuaga na kumuombea katika Kanisa Katoliki Muhimbili jijini Dar es salaam, Sugu amesema kuwa baada ya kuwekwa ndani afya ya mama yake ilibadilika na alianza kuugua shinikizo la damu lililozidisha tatizo alilokuwa nalo awali la figo.

“Desderia alizaliwa Disemba 25, 1956 na maisha yake kwa sehemu kubwa alikuwa mkulima mdogo na amekuwa mjane toka mwaka 1992 baada ya mume wake kufariki na alikataa kuolewa tena na kujikita na shughuli za kanisa,”amesema Sugu

 

Kamanda afunguka kisa cha mtawa kujirusha ghorofa ya tatu
Video: Hamjui Saa wala Siku atakayo kuja Ninja- Lugola